SINGIDA UNITED YAMUACHIA ATHANAS AREJEE STAND UNITED KWA RUHUSA YA SIMBA

Klabu ya Singida United, imemtoa kwa mkopo mshambuliaji wa Simba, Paschal Athanas.

Simba imemtoa Athans kwenda kuichezea timu yake ya zamani ya Stand United baada ya kupata ruhusa kutoka Simba.





Singida United walimchukua Athans kwa mkopo kutoka Simba lakini amekuwa hachezi na Stand United wakaamua kumuomba awaongezee nguvu.



Kwa kuwa ni mchezaji wa Simba, Singida United waliamua kufuata utaratibu wa kuwaomba Simba ambao wamekubaliana na hilo.

Baada ya Athanas kutua Simba alionyesha cheche katika mechi moja tu lakini baada ya hapo, alionekana kuporomoka na hata alipopata nafasi alishindwa kuonyesha kilichotegemewa na wengi.

Post a Comment

0 Comments