BOSI wa Klabu ya AFC Eskelistuna ameshindwa kuwasili nchini wiki
hii kumalizana na Simba kuhusu usajili wa timu hiyo, Said Ndemla baada
ya mmoja kati anayehusika na ujio wake kupata msiba.
Kiongozi huyo alitarajiwa kuwasili nchini wiki hii kwa ajili ya suala la
mchezaji huyo pamoja na masuala mengine ya kisoka lakini imeshindikana.
Ndemla alifanikiwa kufuzu majaribio mwezi uliopita katika klabu hiyo ya Sweden ambayo ilikuwa
inashiriki ligi kuu na sasa imeshuka daraja.
Akizungumza na Championi Jumamosi, meneja wa Ndemla, Jamali Kisongo
alisema kiongozi huyo ameshindwa kuwasili kutokana na matatizo hayo
aliyoyapata mwenzao.
“Yule kiongozi alitakiwa kuwasili nchini wiki hii lakini imeshindikana
kwa sababu mmoja kati ya watu anayehusika na ujio wake amepata msiba,
hivyo sijafahamu baada ya hapo ratiba zake zitakuwaje.
“Lakini kama kutakuwa na lolote tutaweka wazi. Kwa upande wa mchezaji
licha ya timu kushuka daraja lakini dili liko palepale, atajiunga nayo
tu,” alisema Kisongo.
0 Comments