Na John Ndeki
Watu wengi wamekuwa wakijiuliza maswali mbalimbali ambayo yanahusiana na
masuala ya kibiashara. Na miongoni mwa maswali ambayo wamekuwa
wakiniuliza ni kuhusu ni nini faida ya kutangaza biashara kwa sehemu
kubwa?
Swali hili ndilo limenifanya nishike kalamu yangu ili niweze kulijibu.
Nakusihi twende sambamba ili niweze kueleza kwa kinagaubaga, kwa nini
unapaswa kuitangaza biashara yako tena kwa nguvu zote.
Matangazo ni usambazaji wa taarifa sahihi kuhusu bidhaa au huduma
kutoka kwa mfanyabiashara kwenda kwa mteja. Matangazo ndiyo roho ya
biashara, kwani bila kufanya biashara yako bila matangazo ni sawa na
bure.
Nafikiri pia utakubaliana nami ya kuwa ili uweze kufanya biashara yenye
tija ni lazima uitangaze biashara yako, kwani " biashara ni
matangazo". Matangazo ndiyo yatakuyokufanya uweze kuongeza mauzo ya
kibiashara kila wakati.
Kwa kuzingatia hilo unaweza kuitangaza biashara yako kwa njia ambayo
itakuwa ni rahisi kwako. Na sababu kubwa ya kuitangaza biashara yako ni
kuongeza wateja wapya.
Leo na dhumuni kubwa la kutangaza biashara yako ni kukutana na na watu
wapya, ukiona umetangaza biashara yako na hakuna mteja mpya hata mmoja
ujue fika kuna mahala ambapo umekosea.
Hivyo fanya tathimni upya na ujipange upya na kuona ni jinsi gani
unaweza kuitangaza biashara hiyo. Vile vile katika upangaji wa malengo
ya kibiashara hakikisha ya kwamba unapanga na mbinu za kukutana na watu
wapya kila siku.
Nasisitiza juu ya kukutana na watu wapya, kwa sababu nimegundua ya
biashara nyingi zimekuwa hazifanyi vizuri kwa sababu zimekuwa na watu
ambao wanaizunguka biashara ile ni wale wale kila siku. Hivyo kila siku
fanya tathimini juu wateja wapya ambao wamekuja katika biashara yako.
Asante kwa kutembelea mtandao huu wa dira ya mafanikio, usisite kumshirikisha na mwingine ili aweze kujifunza.
0 Comments