Rais wa Tanzania John Magufuli kwa mara ya kwanza katika historia ya
taifa hilo amewasamehe wafungwa 61 waliokuwa wamehukumiwa kunyongwa.
Hata hivyo idadi ya wafungwa wengine walioachiwa huru kutokana na
makossa mbali mbali ni 1,821 ambao amesema kuwa wanapaswa kuachiwa mara
baada ya tangazo lake.
Wafungwa wengine 8157 wamepunguziwa adhabu zao. Idadi hiyo ya msamaha
kwa wafungwa inatajwa kuwa ni kubwa katika awamu zote kuwahi kutokea na
hasa zinazo wahusisha wafungwa wa kunyongwa na vifungo vya maisha.
0 Comments