Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai ametuma
salamu za rambi rambi kwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
Dkt. Hussein Mwinyi pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali
Venance Mabeyo, kufuatia vifo vya askari 14.
Spika Ndugai amesema amepokea kwa masikitiko taarifa za vifo vya askari
hao ambao walikuwa wakilinda amani nchini Kongo, pamoja na wengine 44
waliojeruhiwa kufuatia mashambulizi yanayotekelezwa na askari waasi
nchini humo.
Kufuatia tukio hilo, Spika Ndugai ametoa pole kwa familia za askari hao
waliouawa, na kuwaombea wale waliojeruhiwa kupona haraka na kuendelea na
shughuli za ujenzi wa Taifa.
0 Comments