RASMI,
Shirikisho la Soka nchini (TFF) limetangaza kusimamisha Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara kwa wiki mbili kupisha michuano ya Kombe la CECAFA
Challenge inayotarajiwa kuanza Desemba 3 hadi 17, mwaka huu nchini
Kenya.
Ratiba
mpya iliyotolewa na TFF inaonyesha sasa Desemba 22, 23, 24 na 26,
zitakuwa siku za mechi za kuwania Kombe la Shirikisho la Azam yaani Azam
Sports Federation Cup (ASFC).
Mechi
zitakazochezwa katika siku hizo zitafahamika Desemba 5, mwaka huu
ambako imepangwa droo ya timu 64 zitakazocheza Raundi ya Tatu ya ASFC.
Timu
64 maana yake ni kuwa timu 16 za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara;
timu 24 za Ligi Daraja la Kwanza na timu 24 ambazo zimefuzu kutoka hatua
awali; ya kwanza na pili.
Baada
ya michezo hiyo, ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom itaendelea tena kwa
michezo ya raundi ya 12 itakayofanyika Desemba 29, 30 na 31 kabla ya
ligi kusimama tena kupisha michuano ya Kombe la Mapinduzi.
Michuano ya Kombe la Mapinduzi inatarajiwa kuanza Desemba 30 hadi Januari 13 mwakani visiwani Zanzibar.
0 Comments