AVEVA AHUENI, SASA KESI YAKE KUANZA KUSIKILIZWA MWEZI UJAO


Image result for avens aveva

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa  Tanzania (Takukuru),  imeieleza mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa imeshakamilisha upelezi wa kesi ya Rais wa  Simba, Evans Aveva na makamu wake, Geofrey Nyange 'Kaburu' na wapo tayari  kuanza kusikilizwa.

Aveva leo ameshindwa kuhudhuria tena mahakamani katika kesi  yake utakatishaji fedha inayomkabili ikiwa ni mara ya saba mfululizo kutokana kutokana na kulazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili  kufuatia hali yake ya kiafya kutokuwa nzuri.

Aveva anakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo na kutakatisha fedha  kiasi cha dola 300,000 za Kimarekani akiwa na  makamu wake wa rais Geofrey Nyange 'Kaburu'.

Katika kesi hiyo ambayo itakuwa ikisikilizwa mbele ya   Hakimu Mkazi wa Makahama  ya Kisutu, Thomas Simba badala ya  Victoria Nongwa ambapo wakili wa Takukuru, Nassor Katuga ameiambia mahakama hiyo kwamba kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa lakini wameshakamilisha upepelezi hivyo wapotayari kuendelea kwa hatua ya kuanza kusikilizwa. 

Katuga  alisema kuwa kusema kuwa lakini wapokea taarifa kuwa mshitakiwa namba moja (Aveva) ameshindwa kufika mahakamani kwa kuwa anaumwa na melazwa Muhimbili nabadala yake yupo Kaburu peke yake ambaye ni mshitakiwa namba mbili.

Kwa upande wa  hakimu Simba alisema kuwa ni vyema kufuatilia hali yake kwa kuwa kesi ipo tayari kusilizwa ili iweze kuendana na muda kutona na kuwa ni ya muda mrefu ambapo amepanga kuanza kusilizwa  Aprili 5, mwaka huu.

Post a Comment

0 Comments