SANGA ATOA UFAFANUZI KUHUSU DAN LYANGA...





Mkurugenzi wa Klabu ya Singida United, Festo Sanga, ametolea ufafanuzi wa taarifa zinazoeleza mchezaji wao, Daniel Lyanga amefungiwa kucheza soka na FIFA.


Taarifa zilizozuka leo majira haya ya asubuhi zimeeleza kuwa mchezaji wa Singida United, Lyanga amefungiwa kucheza soka kwa muda wa miezi 6 na sababu zikidai kuwa alisaini mikataba na zaidi ya klabu moja.

Festo Sanga, amesema suala hilo halina ukweli, na mchezaji huyo ni mali yao kwakuwa tayari walishamalizana na Fanja FC ya huko Oman.

Akihojiwa na EFM Radio katika kipindi cha Sports HQ, Sanga ameeleza kinachosubiriwa hivi sasa kutoka Oman ni ITC ya mchezaji, lakini suala la malipo na taratibu zingine zote zimeshakamilika.

Singida United ilimsajili Lyanga kipindi cha dirisha dogo la usajili msimu huu wa 2017/18.

Post a Comment

0 Comments