Bushiri alisema kwamba amefikia makubaliano na uongozi wa Polisi Tanzania kwa ajili ya kwenda kukisaidia kikosi cha timu hiyo ili kifanikiwe kupata nafasi ya kucheza ligi kuu ya Tanzania bara msimu ujao.
Alisema kwamba yeye atakuwa na kazi moja ya kusimamia mechi za timu hiyo ambazo zimesalia na baada ya hapo kama kutakuwa na maelewano mazuri basi atasaini kandarasi ya moja kwa moja kwa ajili ya kuwafundisha maafande hao.

0 Comments