SIMBA
SC imeahidi ushindi dhidi ya wenyeji, Tanzania Prisons katika mchezo wa
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Jumamosi Uwanja wa Sokoine mjini
Mbeya. Mratibu
wa Simba SC, Abbas Suleiman ameiambia john ndeki blog leo
mjini hapa kwamba kikosi kinaendelea vizuri na maandalizi yake mjini
hapa na lengo ni ushindi dhidi ya Prisons. Abbas
amesema baada ya wachezaji waliokuwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya
Tanzania, Taifa Stars kilichotoa sare ya 1-1 na wenyeji Benin mjini
Cotonou Jumapili kuwasili Jumanne, maandalizi yamepamba moto. Amesema
wachezaji wana ari kubwa kuelekea mchezo huo na lengo ni kuendeleza
wimbi la ushindi katika Ligi Kuu baada ya ushindi wa 1-0 katika mchezo
wao wa kwanza mjini Mbeya wiki mbili zilizopita dhidi ya Mbeya City.
Amesema
timu haina majeruhi mpya, ukiondoa wale watatu wa muda mrefu ambao ni
kipa Said Mohammed ‘Nduda’ na mabeki Shomari Kapombe na Salim Mbonde.
Kwa
ujumla baada ya mapumziko ya kupisha mechi za kirafiki za kimataifa
zikiwemo za kufuzu Kombe la Dunia, Ligi Kuu inatarajiwa kurejea kesho
kwa mchezo mmoja tu, Singida United wakiikaribisha Lipuli ya Iringa
Uwanja wa Namfua. Mechi
nyingine za Jumamosi, Ruvu Shooting watakuwa wenyeji wa Ndanda FC
Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani, Stand United n Mwadui FC
Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, Maji Maji na Mbao FC Uwanja wa Maji Maji
mjini Songea na Simba SC dhidi ya Tanzania Prisons Uwanja wa Sokoine
mjini Mbeya. Mzunguko
wa 10 utakamilishwa kwa michezo miwili, Uwanja wa Uhuru mjini Dar es
Salaam, Yanga watakuwa wenyeji wa Mbeya City na Uwanja wa Saba Saba
mjini Njombe, wenyeji Njombe Mji FC wataikaribisha Azam FC. Simba
inaongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 19, sawa na Azam FC inayoshika
nafasi ya pili kwa kuzidiwa wastani wa mabao, wakati Yanga inashika
nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 17, sawa na
Mtibwa Sugar.
0 Comments