Kocha
wa zamani wa timu ya Mwadui FC,Ally Bushiri maarufu kwa jina la "The
Big Boss"amethibitisha taarifa za yeye kujiunga na klabu ya Polisi
Tanzania ambayo inashiliki ligi daraja la kwanza kwa ajili ya
kukifundisha kikosi cha timu hiyo.
Bushiri alisema kwamba amefikia makubaliano na uongozi wa Polisi
Tanzania kwa ajili ya kwenda kukisaidia kikosi cha timu hiyo ili
kifanikiwe kupata nafasi ya kucheza ligi kuu ya Tanzania bara msimu
ujao.
Alisema kwamba yeye atakuwa na kazi moja ya kusimamia mechi za timu hiyo
ambazo zimesalia na baada ya hapo kama kutakuwa na maelewano mazuri
basi atasaini kandarasi ya moja kwa moja kwa ajili ya kuwafundisha
maafande hao.
0 Comments