Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia
ameshinda nafasi ya Ujumbe wa Kamati ya Utendaji katika Baraza la Soka
la Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
Katika uchaguzi huo uliofanyika leo Desemba 2, 2017 jijini Nairobi, Kenya Rais Karia alipita bila kupingwa kuwa Mjumbe CECAFA.
Awali kinyanganyiro hicho kiliwavutia wanachama wanane kabla ya watatu kujiondoa na hivyo watano hao kuchaguliwa bila kupingwa.
Wajumbe hao ambao wataungana na Rais wa CECAFA, Mhandisi Mutasim Gafar
wa Sudan watakuwa na kibarua kuboresha utenda kazi wa baraza hilo kwa
ajili ya kuimarisha soka ukanda huo.
Wengine waliochaguliwa ni Abdiqaani Arab Said (Somalia), Aimable
Habimana (Burundi), Juneid Basha Tilmo (Ethiopia) na Mwanamke Petra
Dorris wa Kenya.
0 Comments