Dar es Salaam. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
kimempongeza Rais John Magufuli kwa kutekeleza ahadi zilizotolewa na
mgombea urais wa chama hicho, Edward Lowassa ikiwemo ya kuwaachia huru
wanamuziki Nguza Viking na Johnson Nguza ‘Papii Kocha’.
Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi na chama hicho imeeleza kuwa katika
ahadi zake Lowassa aliahidi iwapo Chadema ingeshinda uchaguzi
angewaachia wanamuziki hao.
Vilevile chama hicho kimetoa wito kwa Serikali kutumia mamlaka yake
kwa mujibu wa sheria kuondoa nia ya kuwashtaki masheikh wa Zanzibar na
mahabusu na washtakiwa wa makosa ya mtandao.
Ombi hilo pia limewagusa mahabusu wa makosa ya kisiasa, ikiwemo kesi za
uchochezi zinazohusisha kumkosoa Rais, chama na serikali yake.
Mwananchi:
0 Comments