Kitua cha Msaada wa Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimempongeza Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutoa
msamaha kwa wafungwa 8,157 ikiwemo familia ya msanii Nguza Viking.
Pamoja na pongezi hizo LHRC, imesema itaendelea kumuomba Rais Magufuli
abadili baadhi ya sheria ikiwemo kuondoa sheria inayotoa ruhusa ya
adhabu ya kifo..
“Tunampongeza Mh. Rais Magufuli kwa kutoa msamaha kwa wafungwa 61 kati
ya wafungwa 522 waliohukumiwa kunyongwa”. LHRC wameandika kupitia
ukurasa wao wa Twiiter.
Rais Magufuli ametoa msamaha huo leo kwenye sherehe za maadhimisho ya
miaka 56 ya Uhuru wa Tanganyika zilizofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri
mjini Dodoma.
LHRC imeongeza, “Tunamsihi Mhe. Rais kusimamia mabadiliko ya sheria ili
kufuta sheria zinazoruhusu uwepo wa adhabu ya kifo na kuifanya hukumu ya
kifungo cha maisha kuwa adhabu mbadala”.
Katika msamaha huo Rais pia amemsamehe mzee Mganga Matonya ambaye ana
miaka 85 akiwa amekaa gerezani miaka 37 pamoja na miaka saba aliyokaa
mahabusu wakati akisubiri hukumu yake hivyo kufanya afikishe miaka 44
gerezani.
0 Comments