ALIYEKUWA Mbunge wa Kinondoni kupitia Chama Cha Wananchi (CUF), Maulid
Mtulia amekabidhiwa rasmi kadi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mapema leo
katika ofisi za chama hicho.
YALIYOSEMWA NA ALIYEKUWA MBUNGE WA KINONDONI KUPITIA CUF MAULID MTULIA
MARA BAADA YA KUKABIDHIWA KADI YA CCM LEO JUMATATU TAREHE 04/12/2017
“Nimejivua nyadhifa zangu zote ya Ubunge wa Kinondoni na vyeo vyote
nilivyokuwa navyo CUF na kuamua kujiunga na CCM kutokana na kuridhishwa
na CCM ya sasa na utendaji wa Rais Dk. Magufuli.
“Mimi ni mgeni na salamu ninayoijua ya CCM ni CCM Oyeee. Nimejiunga na
CCM ili kuunga mkono kazi nzuri inayofanywa na Rais Dk. Magufuli.
Nimetoka kwenye chama chenye migogoro mingi, nimekuja kwenye chama
chenye amani, haki na Demokrasia ya kweli. Ningekuwa Mbunge kupitia CCM
ningefanya mengi makubwa zaidi,” alisema Mtulia.
“Sijaja CCM kutafuta cheo bali nimetumia haki yangu ya kidemokrasia ya
kujiunga na chama chochote kile ninachokitaka. Kila jambo nililokuwa
namwomba Rais tena hadharani (mfano wakati wa ufunguzi wa maghorofa)
ameyatekeleza kwa kiwango kikubwa.
“Nawashangaa Viongozi wa Upinzani wanaopinga na kususa mambo ya Serikali
na shughuli za Bunge, hizo shida za Wananchi Nani atawatatulia endapo
wanawasusia wenye mamlaka? Nipo tayari kuwa hata Balozi wa nyumba kumi
na ikishindikana nitaenda kuvua samaki nyumbani Rufiji.
“Nawahaidi wana CCM watafurahia uwepo wangu na watanufaika nami ndani ya
CCM. Nawaambia wana Kinondoni wasikosee, wachague Mbunge anayetokana na
CCM. Wachague CCM siku zote,” alisema Mtulia
IMETOLEWA NA;
Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi
UVCCM Taifa.
0 Comments