Yamkini
umeshawahi kusikia kwamba wanaume hukosa uaminifu kwa sababu za kimwili
zaidi wakati wanawake nao hukosa uaminifu kwasababu za kihisia.
Nikweli
kuwa upo ukweli katika hilo, ingawa katika utafiti huu wanawake
mbalimbali walipoulizwa kwanini walijiingiza katika mahusiano yasiri
mbali na wapenzi wao walikuwa na sababu tele zakuelezea, wako
walioelezea kuwa walikuwa wanafurahisha hisia zao tu na wengine walikuwa
kwenye mkakati wakulipiza kisasi kwa kile walichowahi kufanyiwa na
wapenzi wao, na sababu nyingine nyingi zilielezwa.
Jaribu
kusoma kwa umakini ili ufahamu nini walikisema na kilichowafanya
kujiingiza katika majaribu hayo. Ni matumaini yangu kwamba utakutana na
sababu nyingine ninazokusibu au zilizowahi kukusibu wewe, na yamkini pia
ukapata kufahamu kwanini mambo fulani yanaendela vile yalivyo. Kukosekana kwa mvuto Mmoja
wa waliohojiwa anasema “Nilikuwa na mpenzi wangu kwa muda wamiaka
mitatu, alikuwa kijana mzuri sana na nilifurahia sana ninapokuwa naye
lakini tatizo nikwamba hakukuwa na chembe ya mvuto baina yetu. Wengi wa
marafiki zetu walikuwa wameshachumbiana na kuvishana pete lakini kila
mchumba wangu alipojaribu kuanzisha hoja ya kunivisha pete nilijitahidi
sana kubadilisha mazungumzo ili tu tusiklizungumzie hilo.
Ipo
siku nilisafiri kikazi na huko nikakutana na na kijana mfanyakazi
mwenzangu ambaye taratibu nilijikuta naanza kuvutiwa nae. Kwakweli
ulikuwa wakati mzuri sana, labda kwasababu niliitarajia safari hii kwa
muda na nilikuwa sijasafiri kwa muda pia na ukizingatia nimekutana na
mtu ninaevutiwa nae basi mambo yalikuwa mazuri zaidi.
Wakati
wa kurudi ulipofika nilirudi nyumbani nikatengana na mchumba wangu na
kujikuta sasa naanza mahusiano rasmi na yule kijana niliyefanyanae kazi
kule nilikoenda. Ingawa siwezi kusema najisifia kwa nilichokifanya,
lakini namshukuru Mungu kwamba mambo yaliendelea kuwa mazuri upande
wangu kwa sababu mimi na yule kijana tuliamua kuoana na hadi sasa
tunaishi kwa furaha na mapenzi mazuri”.
Kuchelewesha kitendo cha kuachana “Kabla
tu sijaenda kuachana na mwanaume aliyekuwa mpenzi wangu, niligundua
kuwa alikuwa na hali mbaya sana kihisia, hakuwa tayari kabisa kusikia
kwamba tunaachana nahii ikanifanya kukosa ujasiri wa kumtamkia kuwa
tuachane. Kwahiyo nikasubiri kama mwezi mmoja hivi ili haliyake irudi
kuwa njema ndiyo nimwambie.
Mara
tu haliyake ilipokuwa sawa na wakati na mimi nimeshaanza kupata ujasiri
wa kumwambia mara akafukuzwa kazi, nikajihisi tena nimerudi katika
hatua ya kwanza. Wakati huo sasa tayari nilishakutana na kijana ambaye
nilishatamani sana kuanza naye mahusiano, na kwa kushindwa kujizuia na
kwahali niliyokuwa napitia kimahusiano nikajikuta nimemruhusu awe mpenzi
wangu, pasipo hata kumhusisha mpenzi wangu wa awali kuwa sasa nipo
katika mahusiano mengine.
Nahisi
nilijipamoyo kwamba siwezi kumwambia sasahivi wakati hali yake
yakihisia haikuwa nzuri”. (Binti aliyehojiwa hapa alikuwa na miaka 30,
wakati yule wa kwanza alikuwa na miaka 33) Madhara ya kuwa mbali na mpenzi wako “Mimi
na mchumba wangu tuliamua kuendelea na mapenzi yetu tukiwa mbalimbali
mara tu nilipopata nafasi ya kwenda chuo kikuu mbali na nyumbani. Miezi
michache ya kwanza haikuwa na shida, kila kitu kilikuwa sawa na
tuliwasiliana bila shida.
Lakini
kila muda ulipokuwa ukienda nikajikuta naanza kuvutiwa na kuwa karibu
na kaka mmoja aliyekuwa mwanafunzi mwenzangu na mara kwa mara nilikutana
naye maabara za sayansi. Baada ya masomo kumalizika nilirudi nyumbani
na nilimkuta mchumba wangu akinisubiri kwa hamu sana. Kwakweli kukaanae
kipindi hiki haikuwa rahisi kabisa ingawa sikuweza kuachana nae wakati
huu sababu bado nilivutiwa nae.
Ziko
nyakati hapa katikati nilimtembelea yule mwanafunzi mwenzangu
niliyevutiwa nae tukiwa chuoni na nikagundua kuwa kilichokuwa baina ya
mimi na yeye kilikuwa ni hisia zaidi nasio penzi haswa, ingawa
tulishajikuta tukiingia katika penzi, nahisi hii yote ilisababishwa tu
na upweke na kuwa mbali na mwenzangu, basi nikaamua kuacha kabisa
kuwasiliana na yule mwanafunzi mwenzangu na kuweka mawazo yangu yote kwa
mpenzi wangu kwasababu nilijua kuwa yeye ndio alikuwa wangu wa maisha,
nasikitika kwamba sikuwahi kumwambia kilichoendelea wakati nikiwa
chuoni, ingawa maranyingine najihisi kushtakiwa moyoni. Maranyingine
najipa moyo kwamba ule ulikuwa utoto na ujinga tu. Sasa mimi nayeye
tunaendelea vema na ni miaka mine sasa tangu nimemaliza chuo kikuu”.
Kuepukana na kuwa mpweke Binti
huyu mwenye miaka 28 anasema “Nilianza tu kuhusiana kimapenzi na kijana
niliye naye sasahivi mara baada ya kuachwa na mpenzi niliyekuwa naye
kwa miaka miwili.
Kwakweli
ilikuwa ngumu sana kwangu na huyu mpenzi wa sasa kweli aliniokoa katika
maumivu hayo, baada ya mimi nayeye kuwa katika mahusiano kwa miezi
mitano hivi, mpenzi wangu wa kwanza akarudi na kuomba nimruhusu na kumpa
nafasi tena na kuahidi kuwa hayatotokea tena. Ukweli ni kwamba bado
nilihisi kumkosa sana moyoni mwangu, kwahiyo tukaanza kuonana mara kwa
mara ingawa sio kwamba nilikuwa nimeachana na huyu niliyekuwa naye sasa.
Najihisi
nilikuwa nimemuweka huyu kijana wa sasa karibu ili kujihakikishia
usalama zaidi maana sikuwa nikijiamini sana kuwa na yule wa awali,
nilihofia kama ataniacha tena angalau ninamtu pembeni yuko tayari kwa
ajili yangu, ingawa sio kwamba nilimpenda kiukweli kama mpenzi wangu wa
mwanzoni.
Kwa
bahati mbaya mimi na mpenzi wangu wa awali hatukuweza kuendelea vema
hata baada ya kumpa nafasi ya pili aliyoiomba, mbaya zaidi nikwamba
mpenzi wangu wa sasa alipogundua kuwa nilikuwa ninaonana mara kwa mara
na yule wa kwanza na yeye akasema hatoweza kuendelea na mimi. Kweli
nilijifunza somo hapa kuhusu kuhusiana na wanaume wawili wakati mmoja,
na pia kujifanya najaribu kulea nakubembeleza penzi lililokwisha kufa”. Kutafuta pumziko baada ya mahusiano mabaya “Nilipokuwa
binti mdogo (sasa hivi nina 30) nilikuwa katika mahusiano na kijana
mmoja ambaye kwakweli alikuwa akinipinga katika kila ninachokifanya,
alinikejeli sana kuhusu maumbile yangu na uzito wangu, mara aseme mimi
mjinga, mara sijui kitu, mara mi mshamba na mambo mengine mengi mabaya.
Pamoja
na mabaya yote haya bado niliamua kuwa naye tu ingawa marafiki zangu
wote na wazazi na ndugu zangu walimchukia. Siku moja nikiwa kwenye
sherehe nikakutana na kijana mmoja na gafla tulijikuta tumezama kwenye
maongezi ya mapenzi na hisia zetu kuvaana. Yani huyu alikuwa ni tofauti
kabisa na mpenzi wangu, wametofautiana kilakitu kuanzia maneno hadi
matendo, yani ni kijana mpole, mzuri wa tabia, mkarimu na ananitia moyo
badala ya kunivunja moyo.
Mara
kwa mara tulikuwa wote tukifurahia siku za mwisho wa wiki,na moyoni
mwangu ikawa kama vile taa ya yule wa kwanza ndiyo imezima kabisa. Kwa
mara ya kwanza nilimbusu usiku kabla hajaondoka kurudi nyumbani kwao, na
nilipoenda kuonana na yule wa kwanza nilimwambia tuachane. Niliamua
kuendelea sasa rasmi katika mapenzi na mpenzi wangu mpya na baada ya
miaka mitatu tukaamua kuoana”.
Jitihada za kutafuta kile unachohisi kukikosa “Mimi
ni binti niliyekulia katika mikoa ya pwani kwahiyo napenda sana kwenda
fukweni kukaa, kuogelea na kupunga upepo. Kwa bahati mbaya mpenzi wangu
amekulia zaidi bara kwahiyo mambo ya fukweni kwake sio kitu kabisa na
hapendi, mara kwa mara tumekuwa na ushindani na mikwaruzano kuhusu wapi
twende tukapumzike na mara zote yeye ndio anashinda.
Baada
ya kuwa kwenye mahusiano kwa muda wa miezi nane, kuna wakati nilisafiri
mimi na rafikizangu na tulitumia boti kwa muda mrefu wa safari, nahodha
wa boti hii alikuwa kijana mzuri, mtanashati na anaonekana ni mtu wa
maisha ya fukweni zaidi, kweli nilivutiwa nae, Tulipofika tuliahidiana
kuonana usiku ule na tulikuwa na wakati mzuri sana pamoja, sikuwahi
kumwambia mpenzi wangu kuhusu yaliyoendelea katika safari yangu, na wala
sijihisi kushtakiwa moyoni mwangu, tena kuna maranyingine najihisi
ndani yangu kuwa kile ndicho kilikuwa chema kumfanyia huyu mpenzi wangu
kwasababu ya utukutu wake.
Bahati
mbaya sana mimi na mpenzi wangu hatukuweza kuendelea sana, tuliachana
baada ya mimi kushindwana naye na niliamua kuhakikisha kwamba kila
kijana nitakayeamua kuhusiana naye basi lazima ayajue maisha ya
fukweni”.
Jitihada za kumuadabisha (kumkomesha) “Mpenzi
wangu wa mwisho alikuwa na tabia za wanawake sana kabla hatujaamua
kuanza neye mahusiano, nilidhani ningeweza kumbadilisha tabia yake hiyo
lakini nilijidanganya, mara kwa mara nilisikia tetesi kuwa alikuwa
anaonana na wasichana wengine wakati bado tuko naye katika mahusiano,
lakini kila nilipomuuliza marazote alikataa katakata.
Usiku
mmoja nilipata simu kutoka kwa msichana ambaye walikuwa wamehusiana
naye kwa miezi mitatu na akaniambia kuhusu msichana mwingine pia ambaye
na yeye amegundua kuwa anamahusiano na huyu mpenzi wangu. Nilikuwa na
hasira sana usiku ule, niliamua kutoka na marafiki zangu nikiwa
nimevalia mavazi ya kumvuta kila mwanaume ambaye aliniona, na nikaamua
kuwa na muda na kijana fulani mzuri sana niliyekutana naye katika mtoko
ule.
Ndani
yangu nilipata kupumua kidogo nikajihisi kuwa angalau hicho ndiyo
alichostahili mpenzi wangu huyu, nilitamani na nilifurahia kuuona uso
wake jinsi anavyokuwa wakati nikimpa taarifa ya nilichokifanya usiku ule
na ninayoyajua kuhusu yeye na wanawake zake na hatimaye nikamwambia
kila mtu achumue muda wake, na tukaachana”.
0 Comments