Zijue njia za kujikinga na UTI kwa wanawake na wanaume




Kunywa maji na vinywaji kwa wingi kila siku. Hii itakusaidia ukojoe mara kwa mara na kuruhusu backeria kujenga makazi kwenye njia ya mkojo. Kojoa kila ujisikiapo mkojo na usibane kwa muda mrefu.

Njia za kujikinga na UTI kwa wanawake.
1.    Nenda ukakojoe mata tu umalizapo tendo la kujamiana. Hii itasaidia kutoruhusu backeria kuingia na kujenga makazi kwenye njia ya mkojo.

2.    Badili pedi mara kwa mara uwapo hedhini.

3.    Epuka kujisafisha ukeni na maji yarukayo kwa kasi, pia epuka kupulizia marashi ukeni, ama kutumia pedi zenye kemikali za kukata harafu. Hizo huuana backeria wa asali wa ukeni hali ambayo hukaribisha backeria wa maradhi kuzaliana kwa wingi.

4.    Ujisafishapo baada za kujisaidia anzia mbele kwenda nyuma kuepusha kuhamisha backeria walio eneo la haja kubwa kuingia njia ya mkojo.

5.   Kwa wale  walio katika kipindi chao cha ukomo wa hedhi, waweza kushauliana na dakatari juu ya kutumia oestrogen ya ukeni  kuwasaidia kujikinga na maambukizi.

Mbinu za kujikinga  na UTI
1.    Hakikisha maeneo ya nncha ya sehemu zako za siri ni masafi muda waote.

2.     Tumia kondom wakati wa kufanya tendo la ndoa ni kinga nzuri kwa ajili ya maambukizi ya ugo jwa huu.

Post a Comment

0 Comments