Necta yafanya mabadiliko mtihani darasa la saba

Image result for wanafunziBaraza la Mitihani la Taifa, (Necta) limefanya mabadiliko ya mfumo wa utungaji wa mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi.
Mabadiliko hayo yametangazwa na Mtendaji wa Baraza hilo, Dk Charles Msonde, na kusema kwamba muundo wa mitihani hiyo umebadilishwa na kamati iliyohusika kufanya mabadiliko hayo imeafikiana kwamba katika kila somo kutakuwa na maswali 45.
Ambapo kati ya hayo maswali 40 yatakuwa ya kuchagua jibu sahihi na 5 yasiyo ya kuchagua yatakuwa ni maswali ya kujieleza, kuonyesha njia na jibu sahihi.
Ameongezea kuwa maswali hayo 40, katika kila swali litakuwa na alama moja na maswali matano kila swali litakuwa na alama mbili huku majibu ya maswali 40 yatajibiwa kwenye fomu ya OMR, na maswali 5 yatajibiwa kwenye karatasi maalumu itakayoandaliwa.
Kufuatia muundo huo mpya Necta imetoa wito kwa walimu wakuu kuanza kuwapima wanafunzi kwa kutumia mabadiliko hayo ili kuwajengea uzoefu.Baraza la Mitihani la Taifa, (Necta) limefanya mabadiliko ya mfumo wa utungaji wa mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi.
Mabadiliko hayo yametangazwa na Mtendaji wa Baraza hilo, Dk Charles Msonde, na kusema kwamba muundo wa mitihani hiyo umebadilishwa na kamati iliyohusika kufanya mabadiliko hayo imeafikiana kwamba katika kila somo kutakuwa na maswali 45.
Ambapo kati ya hayo maswali 40 yatakuwa ya kuchagua jibu sahihi na 5 yasiyo ya kuchagua yatakuwa ni maswali ya kujieleza, kuonyesha njia na jibu sahihi.
Ameongezea kuwa maswali hayo 40, katika kila swali litakuwa na alama moja na maswali matano kila swali litakuwa na alama mbili huku majibu ya maswali 40 yatajibiwa kwenye fomu ya OMR, na maswali 5 yatajibiwa kwenye karatasi maalumu itakayoandaliwa.
Kufuatia muundo huo mpya Necta imetoa wito kwa walimu wakuu kuanza kuwapima wanafunzi kwa kutumia mabadiliko hayo ili kuwajengea uzoefu.

Post a Comment

0 Comments