Ufahamu Ugonjwa wa Pangusa kwa Undani zaidi





Pangusa  ni ugonjwa wa zinaa unaoambukizwa kwa njia ya ngono. Pia huambukizwa na bakteria anayefahamika kitaalamu kama haimophilus ducrey.

bacteria huweza kupita kwenye ngozi laini kama ya uke kirahisi bila hata kuwepo kwa michubuko. Wanawake huweza kuhifadhi bacteria hawa bila kuonyesha dalili yeyote na kuwaambukiza waanaume wengi zaidi. Ugonjwa huu huleta vidonda vikubwa sana kwenye sehemu za siri na kusababisha kulika kwa sehemu hizo,Pia huweza kuzimaliza kabisa sehemu za siri kama matibabu yasipopatikana.

Ugonjwa huu hupatikana kwenye sehemu za joto na wagonjwa wengi ni wanawake wanaojiuza hasa sehemu za mijini. Ugonjwa huu hurahisisha zaidi maambukizi ya virusi kwa ukimwi kwa waathirika wa ugonjwa huu, baada ya kuambukizwa mgonjwa huchukua siku 3 mpaka 14 kuanza kuonyesha dalili.

Dalili za ugonjwa wa wa pangusa..
Baada ya maambukizi vipele hutokea kisha huchimbika na kutoa vidonda vikubwa ambavyo husambaa pande mbalimbali za sehemu za siri na kuchimba mashimo ya vidonda. Vidonda hivi hua na maumivu makali na hutoa damu pale vinapoguswa.
hali hua mbaya zaidi kwa waathirika wa ugonjwa wa ukimwi.

Vipimo vinavyofanyika, daktari mzoefu anaweza akagundua ugonjwa huu bila vipimo vyovyote lakini kwa uhakika zaidi majimaji yanayotoka sehemu za siri huchukuliwa na kupimwa maabara.

Matibabu ya ugonjwa huu.
vidonda vinatakiwa viweke visafi, vioshwe na sabuni mara kwa mara
dawa zinazotumika kutibu shida hii ni kama cotrimoxazole, ciproflaxin na erythromycin.

Jinsi ya kuzuia ugonjwa huu.

1.      Matumizi ya kondom kwa usahihi.
2.      kua na mpenzi mmoja muaminifu.
3.      Usishiriki ngono kabisa kama huwezi kutumia kondomu.
4.      Epuka wapenzi wengi


Post a Comment

0 Comments