Endometriosis ni ugonjwa wa wanawake ambao tishu zinazotengeneza ukuta wa ndani wa mfuko wa uzazi hukua sehemu ya nje ya mfuko wa uzazi. Sehemu ya ndani ya ukuta wa mfuko wa uzazi huitwa "endometrium" kwa lugha ya kimombo.
Endometriosis hutokea wakati ukuta wa ndani wa mfuko wa uzazi unapokua juu ya mfuko wa mayai ya uzazi (ovary), utumbo, na tishu zilizopo kwenye mifupa ya kiuno (pelvis). Si kawaida kwa tishu za endometrial kuenea zaidi ya eneo la mifupa ya kiuno (pelvic), na huwa haiwezekani kutokea. tishu zinazokua ndani ya ukuta wa mfuko wa uzazi (Endometrial) na zinazoota au kukua nje ya mfuko wa uzazi (mji wa mimba) huitwa "endometrial implant" kwa lugha ya kimombo.
Dalili hizi ni:
1. Maumivu
- Maumivu makali kabla au baada ya hedhi
- Maumivu makali wakati wa tendo la ndoa
- Maumivu ya tumbo, mgongo na maeneo ya mifupa ya kiuno (pelvis)
- Maumivu unapotaka kwenda kujisaidia/kwenda haja
- Maumivu ya miguu
2. Hedhi
- Kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi, damu hiyo inaweza kuwa au kutokuwa na mabonge
- Kuwa na hedhi ya muda mrefu isivyo kawaida
- Kupata hedhi kabla ya muda wa kawaida
3. Uke
Maumivu makali wakati wa tendo la ndoa
4. Matatizo ya Kibofu na Utumbo
- Kutokwa na damu maeneo ya Kibofu au Utumbo
- Kubadilika kwa hali ya utumbo i.e Kuwa na haja kubwa ngumu (constipation) na Kuharisha
- Kukojoa mara nyingi isivyo kawaida
5. Kuvimba kwa tumbo wakati wa hedhi, kwaweza kuwa na maumivu au bila maumivu
6. Kuishiwa nguvu au uchovu wakati wa hedhi
0 Comments