USHINDI
wa 1-0 dhidi ya Njombe Mji FC, unaashiria Azam FC imedhamiria kweli
kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu.
Azam
FC imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Njombe Mji FC leo
Uwanja wa Saba Saba mjini Njombe, bao pekee la Nahodha, Aggrey Morris
kwa penalti dakika ya 60 baada ya winga Mghana, Enock Atta Agyei
kuangushwa kwenye boksi.
Azam
FC sasa inafikisha pointi 22, sawa na Simba SC lakini inaendelea
kukamata nafasi ya pili kutokana na kuzidiwa na wastani wa mabao (GD) na
Wekundu wa Msimbazi.
Wote, Azam FC na Simba wanawazidi kwa pointi mbili mabingwa watetezi, Yanga SC baada a raundi 10 za Ligi Kuu msimu huu.
Mtibwa
Sugar waliouanza msimu vizuri na kuongoza kwa takriban raundi tano, leo
wameanza kujitoa taratibu kwenye mbio za ubingwa baada ya kichapo cha
1-0 kutoka kwa ndugu zao, Kagera Sugar Uwanja wa Manungu, Turiani,
Morogoro.
Bao
pekee la Kagera Sugar limefungwa na kiungo mshambuliaji Edward
Christopher Shijja dakika ya 84 kwa penalti, baada ya beki Dickson Daudi
Mbeikya kuunawa mpira uliopigwa na Jafar Kibaya.
Mtibwa
sasa wanabaki na pointi zao 17 baada ya mechi 10, wakati Kagera Sugar
iliyoanza vibaya inajivuta juu hadi nafasi ya 10, ikifikisha pointi 10
sawa na Ndanda FC baada ya mechi 10 pia.
Njombe
Mji FC inabaki na pointi zake saba katika nafasi ya 15 kwenye Ligi Kuu
ya timu 16, mbele ya Stand United yenye pointi sita, nyuma ya Ruvu
Shooting yenye point inane, sawa na Mbao FC na Mwadui FC yenye pointi
tisa.
0 Comments