Katika hali ya kushangaza watu walijua katizo hilo ni la jana tu kama ilivyotangazwa lakini leo pia, Umeme umekatika ghafla na TANESCO tayari wametolea maelezo ya katizo hilo la umeme kwa siku ya pili kupitia kwenye tovuti yao taarifa hiyo imesomeka kama ifuatavyo.
Shirika la Umeme Tanzania linawataarifu Wateja wake kuwa wakati Wataalamu wetu wanaendelea kurekebisha mifumo yetu ya grid kutokana na hitilafu iliyotokea jana, Imegundulika mifumo ya Gridi haijatengemaa vizuri na hivyo wanaendelea na kazi kuhakikisha huduma ya umeme inarejea.
0 Comments