WINGA
wa Fanja ya Oman, Daniel Lyanga amesema kwamba anaamini ana uwezo wa
kuchezea timu ya taifa ya Tanzania, lakini anaheshimu maamuzi ya kocha
wa Salum Shaaban Mayanga.
Akizungumza
na JOHN NDEKI =online kwa simu kutoka Muscat, Oman jana,
Lyanga alisema kwamba anaamini wakati utafika naye ataitwa kutoa mchango
wake Taifa Stars.
“Hayo
ni maamuzi ya kocha, maana yeye ndiye anachagua na anaona wapi panamfaa
nani na wapi panamfaa nani. Na mimi sina tatizo na hilo, kwa kuwa
wanaoitwa pia ni wachezaji kama mim na mimi itafika tu zamu yangu kama
itatokea nafasi ya kuitumikia Taifa Stars nitaitwa kuitumikia,”amesema.
Lyanga
ni kiungo mshambuliaji tegemeo wa Fanja kwa sasa ambaye alijiunga na
timu hiyo ya Muscat Septemba mwaka jana akitokea Simba SC ya Dar es
Salaam, ambayo nayo ilimrudisha nyumbani Tanzania kutoka Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo (DRC) alipokuwa akichezea Daring Club Motema Pembe
(DCMP) ya Kinshasa mwaka 2015.
Tangu
Septemba mwaka jana, Lyanga aliyekwenda Kongo akitokea Coastal Union ya
Tanga, amecheza mechi 26 na kufunga mabao saba, huku akiseti mabao 12
kwa krosi zake maridadi.
“Huku
ninacheza sana winga zote mbili, kushoto na kulia ndiyo wananitumia
sana japo msimu wa mwaka jana nilicheza namba zote za mbele
hapo,”amesema.
Katika
klabu hiyo, Lyanga anacheza pamoja nyota wengine wawili aliowahi
kucheza nao Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, viungo Mkongo Mbuyu Twite
aliyekuwa Yanga na Muivory Coast, Kipre Michael Balou aliyekuwa Azam
FC, ambao wote wanaweza kucheza kama walinzi pia.
“Nipo nao wote huku na wote tunamshukuru Mungu tupo kama wachezaji muhimu kwenye timu, tunafurahia maisha,”amesema.
0 Comments