Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Mhe.Samia Suluhu Hassan
amezindua kampeni ya Uzalendo na Utaifa 'Nchi Yangu Kwanza' itakayokuwa
ikifanyika kila mwaka sambamba na maadhimisho ya kifo cha Baba wa
Taifa.
Kampeni hiyo iliyoandaliwa na Wizara Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
kwa kushirikiana na Taasisi ya Mpoto Thearte Gallary ina nia
kukumbushana suala la uzalendo ikiwemo kuepusha rushwa, maadili ya
viongozi wa Umma pamoja na kukufua uwajiikaji kwa watumishi wa umma.
Makamu wa Rais amemuomba Waziri Dkt.Mwakyembe aunde kamati ndogo itakayozunguka katika maeneo yote ya nchi kuhamasisha uzalendo.
" Uzalendo siyo kipaji bali unajengwa na kuaandaliwa na jamii husika,
kampeni hii inatoa fursa ya kuelimisha vijana umuhimu wa
tamaduni,sanaa,mila na maadili ya kitanzania. Tufanye mambo kwa wakati ,
wakati tunawakati ,tuutumie wakati vizuri kutekeleza mambo yetu,"
alisema makamu wa Rais " Makamu wa Rais .
Kwa upande wa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka watanzania kuwa
wazalendo kwa kupenda mila na tamaduni za ndani kwa kuwa hizo ndio alama
ambazo zinaitambulisha nchi na kuzitofautisha na mataifa mengine.
"Tuwe wazalendo kwa kupenda sanaa na tamaduni zetu zinazotutambulisha
sisi kama taifa, ufanye kazi kwa bidii ili tuzalishe mali kwa wingi na
kujenga taifa letu huo ndio uzalendo," Waziri Mkuu Mhe.Majaliwa
"Tunayosababu ya Kumuunga mkono Mhe.Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika
kuwahamasisha watanzania kuwa wazalendo. Suala la uzalendo kwa nchi
yetu siyo jambo geni hivyo ni wajibu wetu kuudumisha kwa maslahi ya
taifa letu na ili kufikia uchumi wa viwanda ni wajibu wetu kuwa
wazalendo kwa kusimamia rasilimali zetu," aliongeza Majaliwa.
Naye Waziri wa Habari Dkt Mwakyembe alisema uzalendo ni kuthamini vitu
vyetu pamoja na lugha ya kiswahili amayo imekuwa kivitio duniani kote.
"Kufikia 2063 kiswahili itakuwa lugha kuu barani Afrika na utambulisho
wa mtu mweusi, huo ndio uzalendo na maendeleo ya Sayansi na teknolojia
katika Tehama imesababisha misingi bora ya utamaduni wetu kupata
nyufa"Dkt.Mwakyembe.
Waziri amewataka watanzania kuipokea kampeni hiyo kwa mikono miwili kwa
kuwa ni kampeni ambayo inaenda kulifanya taifa la watu ambayo wapo
tayari kufa kwaajili ya nchi yao.
Katika usiku huo wasanii wakiongozwa na Mrisho Mpoto waliimba wimbo
maalum kwaajili ya kampeni hiyo. Wasanii hao ni pamoja na Fid Q, Ray C,
Witnes, Kassim Mganga pamoja na wengine.
Attachments area
0 Comments